• This is default featured slide 1 title

    Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

  • This is default featured slide 2 title

    Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

  • This is default featured slide 3 title

    Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

  • This is default featured slide 4 title

    Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

  • This is default featured slide 5 title

    Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

Wednesday, November 8, 2017

UMUHIMU WA KUVAA SOKSI .

 


So after a long pause here we are....November kama tunavoiona joto kali sana kwa baadhi ya mikoa.Topic zetu za sasa zitaendana na mabadiliko ya hali ya hewa ya sasa. Miguu ni sehemu mojawapo inayotoa jasho  sana hivvo ni vema kuiweka mikavu kuzuia ukuaji wa bacteria au fungus.Wakaka tunajua umuhimu wa soksi au tunavaa bila kujua na wengine hatuvai? Hii ni kwa wadada pia wanaovaa viatu kama raba au hata nyumbani. Ni vema sana kufahamu kwanini tunavaa soksi na mda mwingine soksi gani tuvae.

1.KUZUIA MAGONJWA YA NGOZI MIGUUNI.

Tumia sekunde tatu tu kuvaa soksi na ujikinge na maradhi haya ya fungus na bacteria, kama sio mpenzi was soksi nashauri ufikirie tena maamuzi yako ya kutovaa soksi.

2.EPUKA HARUFU MBAYA YA MIGUU
Image result for atletes foot
Kwa kweli hii ni kero kwako na wanaokuzunguka.Usipovaa soksi jasho lote la miguu litaenda kwenye viatu na ivo viatu kutoa harufu.Soksi hunyonya lile jasho na huzuia harufu iyo. Aya basi tushtuke aibu hii ya nini katika karne ya watanashati sisi.Tuvae soksi na kubadili kila siku.

3.LAINISHA NGOZI YA MIGUU YA YAKO

Nani hapendi miguu soft?? wadada kutwa kusugua miguu saloon.Simple ukirud nyumban kama sakafu ni ngumu vaa soksi zako nyepesi safi miguu iwe laini.Baadhi ya viatu pia vina surface ngumu kwa chini (wakaka) ukiweka soksi zako safi hamna maneno.

4.KUPUNGUZA MAUMIVU MIGUUNI

Hii hasa kwa watoto wadogo ..tuwazoeze mapema kuvaa soksi.Mtoto anatembea ndani Mara akanyage maji mara vitu vya ncha Kali....Pia kuna viatu ukivaa bila soksi lazima upate maumivu na kupata zile sugu nyeusi.

5.KUPATA JOTO NYAKATI ZA BARIDI 

Wale was mikoa iliyo na baridi kwa sasa naamini tuna soksi za kutosha za miguuni na mikono.Kama kuna sehemu inayongoza kutoa joto ni miguuni na mikononi.Basi vaa soksi ili kuzuia joto lisipotee.

6.MVUTO

Ili sio geni, mi mtu akivaa viatu bila soksi kwa kweli napunguza maksi za utanashati...wengine wanasema kuna viatu vya kutovaa soksi. .hakuna kitu kama icho kuna soksi ndogo ambazo hazionekani kwa juu zimejaa tele madukani tutafte.Ebu mtu kavaa kiatu chake safi akiweka na soksi safi inaonekana mvuto lazima uwepo....Nani hapendi kuvutia??basi sote tunapenda tuvae soksi 


Siandiki mengi sana, soksi sio jambo geni, tubadilike tujijali,.Ok unavaa soksi Je?unavaa soksi pea moja mara ngapi, unafua na kukausha vizuri maana soksi mbichi ni janga jingine la uchafu na maradhi.Kitu kingine ujue aina ya soksi nyakati za joto usivae soksi ambazo  ni nzito sana vaa nyepesi, ambazo ni nzito vaa nyakati za baridi. Na soksi za watoto tununue ambazo hazibani sana. Kwa maswali na maoni weka comment hapo chini tutajadili.

Ahsanteni.

Cheers 
chelly





Share:

Friday, September 22, 2017

NJIA TANO ZA KUTOA MADOA KWENYE NGUO ZA NDANI.

NGUO ZA NDANI BILA MADOA NI WAJIBU SIO WITO

Image result for baking powder stain remover
Wote yametukuta kwa njia moja ama nyingine, iwe katika siku zetu au uchafu unaotoka ukeni kama njia moja ya kujisafisha. Ile rangi inayobaki katika nguo ya ndani ni sababu ya kiwango cha acid kilichopo katika uchafu huo.

Sio siri kwa wadada wote menstruation blood (damu ya hedhi) ni adui kwa nguo zetu za ndani hasa unapopata kiajali safarini. Kwahiyo lazima ujue mbinu ya kuondoa stains (madoa sugu na ya kawaida) katika nguo zako za ndani,,huwezi kuchoma kila yenye doa sio?

Twende sawa tuone njia hizi rahisi za kundoa madoa kwenye nguo za ndani:

1. MAJI YA BARIDI.
Suuza nguo yako ( chupi) mara s tu unapoivua au kugundua kama imepata doa lolote iwe hedhi au uchafu wa kawaida. Maji ya baridi yanasaidia kulainisha uchafu na kufanya usigande. Kisha fua kwa sabuni yako ya kila siku.

2.ASPRIN (dawa)
Kama huna vidonge vya asprin nikushauri tu uwe navyo kuanzia sasa, zitakuokoa. Ponda vidoge vichache vya asprin kupata ungaunga kisha changanya na maji kidogo kupata ujiuji, kisha weka uji huo kwenye sehemu yenye doa  kisha uache kwa usiku kucha kisha fua.Wingi wa uji unategemea na ukubwa wa doa katika nguo yako ya ndani.

3. BAKING POWDER
 Image result for baking powder stain remover
Hii ni rahisi, taratibu zake ni kama zilivo katika asprin.Sema hii mi naiamini sana ilinipa majibu murua katika kutoa rangi mbovu kwenye kwapa. Jina jingine ni chapa mandashi.

4.HYDROGEN PEROXIDE.
Hii watu wanatumia kwenye vidonda, pharmacy zipo bei ya kawaida sana.paka kiasi sehem yenye doa au loweka kisha acha kwa mda hata dakika 30 kisha fua kawaida. Inaweza sababisha kuchuja kwa rangi tumia kwa nguo za ndani ambazo hazichuji.

5. LIMAO
Image result for lemon
Huyu ndo masterplan, anapatikana kirahisi ana kazi nyingi sana ikiwemo kuondoa madoa kwenye nguo za ndani. Loweka ngui yako ya ndani kwenye maji ya limao kwa muda kisha fua kawaida.Tumia kwa nguo ambazo hazichuji.


BONUS
  • Napenda kutoa njia nyingi asilia na nyepesi ila zinaitaji kuwa makini na kujenga tabia. kwa wanaopenda artificial unaweza nunua chemicals ambazo zinatoa madoa ILA  usuuze kwa maji mengi baana ya kufua ili kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza.
  • Tumia pantliners zisizo na harufu kipindi ambacho haupo kwenye c pihedhi,,usipozipenda usiendelee kutumia au tengeneza zako nyumbani( topic special)

Haina haja ya kutupa underwears kila siku sababu ya madoa, au kushindwa kuvaa underwear nyeupe kwa sababu hiyo. Naomba wahanga wenzangu mjaribu kisha tupia comment yako hapo chini au kama una swali unahitaji maelekezo namba yangu pia ipo wazi kwa profile.


Ahsante kwa mda wako
chelly
cherrs.

image powered by google
Share:

Thursday, August 17, 2017

ONDOA WEUSI KWENYE KWAPA KWA NJIA ZA ASILI


ONDOA WEUSI KWENYE KWAPA KWA NJIA ZA ASILI


Hello readers ,nimependa kushare hii topic sababu watu wengi wana shauku ya kufahamu jinsi ya kuondoa icho kirangi kwenye kwapa au mapajani tofauti na artificial ways ambazo labda ni gharama, zina madhara au wanaona hazifanyi kazi.Tips zifuatazo ni rahisi sana na zinafanya kazi lakini lazima ufanye kwa muda kidogo ili uanze kupata matokeo angalau wiki mbili kila siku sababu hizi sio kemikali.


1. LIMAO



Hii unaweza kutumia kutoa weuse sehemu yoyote ya mwili,iwe kwenye mapaja au kwapani.Ni rahisi kata kipande cha limao sugua kwapa lako, acha kwa dakika kumi halafu oga. Kumbuka limao inasaidia kutoa harufu mbaya pia kwenye kwapa. Paka mafuta laini au deodorant kuzuia ngozi isikauke.

2. VIAZI MVIRINGO





Hii pia ni bleaching agent kama limao. Lakini viazi ni vizuri zaidi sababu havikaushi ngozi na havisababishi muwasho wowote.Unaweza sugua kwapa na kipande cha kiazi au ukasaga kiazi chako kwa blenda na kujisugua na juisi yake kasha kuoga baada ya dakika kumi.

3. TANGO





Tofauti na kuleta harufu nzuri mdomoni, kuondoa weusi machoni, habari njema ni kwamba ukisugua kipande cha tango sehemu yenye weusi mara mbili kwa siku tatizo hilo huisha.Unaweza tumia na limao au asali kwa pamoja.

4. ZAFARANI





Hiki ni kiungo kinapatikana maduka ya vyakula au sokoni. Ni rahisi kutumia na ina majibu ya haraka na mazuri.Chukua lotion kiasi kisa changanaya na zafarani kiasi kisha paka kwenye kwapa inatoa weusi na kuleta harufu nzuri pia.Waweza tumia kama deodorant pia.

5. BAKING SODA



Lazima hii tunayo nyumbani, ile ya kupikia maandazi, hii itatenda miujiza kama sio maajabu kwa kwapa zako. Rahisi changanya baking soda na maji kidogo kutengeneza uji, paka kwapani au mapajani acha ikauke kabisa ndo ujioshe na maji ya baridi.

6. MAGANDA YA MACHUNGWA



Warembo wangu hii itawafaa, kausha vizuri maganda ya machungwa kwa siku tatu juani.Yatwange au saga kutengeneza poda au ungaunga weka kwa kikopo na funika.Chota vijiko viwili changanya na rose water (inapatikana madukani) paka kwapani. Acha ikauke kwa dakika kumi halafu uoshe na maji baridi. Kwani bafuni tunaweka nini zaidi ya vitu kama hivi? Msimu wa machungwa haujaisha wapenzi.

7. MAZIWA



Wapenzi wa kunywa maziwa siwaoni wakifanya hii…ila ina majibu ya haraka ukifanya kila siku. Paka maziwa kidogo tu kwenye kwapa acha yakauke kwa dakika 15 halafu oga. Fanya hivi kila siku kupata majibu.

8. MAFUTA YA NAZI



Hakuna kitu ambacho mafuta ya nazi hayafanyi!!hata hivyo ni kiungo cha urembo duniani kote.Inafanya kazi taratibu.Hivyo nashauri utumie kila siku. Jisugue (massage) na mafuta ya nazi kwa dakika 15 kabla hujaoga.Wapenzi wa deodorant hii pia ni deodorant ya asili.

9. VINEGAR




Kama msomaji mzuri wa post zangu lazima uwe na vinegar nyumbani mpaka sasa. Ina matumizi mia kidogo, supermarket zote zipo.paka kwapani acha kwa dakika kumi then oga. Inaondoa harufu, inaua bacteria na inatoa weusi.

10.UNGA WA DENGU ( GRAM FLOUR )




Hii inasaidia pia kutoa mabaka ya chunusi, na weusi sehemu zote mwilini ikiwemo kwapa.Changanya na juisi ya limao na yogurt paka kwenye kwapa kila siku and watch the magic happen. Ni salama

11. APPLES.




Apple ina kiwango cha acid pia hivyo ukisugua kwapa na apple lililosagwa inatoa weusi na harufu. Fanya hivi angalau mara moja kwa siku kabla ya kuoga.

12. YOGHURT



Changaya yoghurt vijiko viwili na asali kijiko kimoja kisha paka kwenye kwapa acha ikauke , osha na maji baridi itasaidia kutoa uchafu na weusi kwenye kwapa.


Unaweza chagua njia moja kati ya hizi au unaweza changanya njia mbili kwa wakati mmoja, Njia zote ni salama sana na ni rahisi sababu vitu vyote hivi ni  viungo na vyakula ambavyo tunatumia nyumbani. Kama una swali uliza kwenye comment  au maoni na atakaejaribu njia yoyote atupe majibu yake kwa comments.

xoxo
chelly


image powered by google.





































Share:

Search This Blog

Chaila Mustapha. Powered by Blogger.

Featured Post

UMUHIMU WA KUVAA SOKSI .

  So after a long pause here we are....November kama tunavoiona joto kali sana kwa baadhi ya mikoa.Topic zetu za sasa zitaendana na ...

Recent Posts

Theme Support