ONDOA WEUSI KWENYE KWAPA KWA NJIA ZA ASILI
Hello readers ,nimependa kushare hii topic sababu watu wengi wana shauku ya kufahamu jinsi ya kuondoa icho kirangi kwenye kwapa au mapajani tofauti na artificial ways ambazo labda ni gharama, zina madhara au wanaona hazifanyi kazi.Tips zifuatazo ni rahisi sana na zinafanya kazi lakini lazima ufanye kwa muda kidogo ili uanze kupata matokeo angalau wiki mbili kila siku sababu hizi sio kemikali.
1. LIMAO
2. VIAZI MVIRINGO
Hii pia ni bleaching agent kama limao. Lakini viazi ni vizuri zaidi sababu havikaushi ngozi na havisababishi muwasho wowote.Unaweza sugua kwapa na kipande cha kiazi au ukasaga kiazi chako kwa blenda na kujisugua na juisi yake kasha kuoga baada ya dakika kumi.
3. TANGO
Tofauti na kuleta harufu nzuri mdomoni, kuondoa weusi machoni, habari njema ni kwamba ukisugua kipande cha tango sehemu yenye weusi mara mbili kwa siku tatizo hilo huisha.Unaweza tumia na limao au asali kwa pamoja.
4. ZAFARANI
Hiki ni kiungo kinapatikana maduka ya vyakula au sokoni. Ni rahisi kutumia na ina majibu ya haraka na mazuri.Chukua lotion kiasi kisa changanaya na zafarani kiasi kisha paka kwenye kwapa inatoa weusi na kuleta harufu nzuri pia.Waweza tumia kama deodorant pia.
5. BAKING SODA
Lazima hii tunayo nyumbani, ile ya kupikia maandazi, hii itatenda miujiza kama sio maajabu kwa kwapa zako. Rahisi changanya baking soda na maji kidogo kutengeneza uji, paka kwapani au mapajani acha ikauke kabisa ndo ujioshe na maji ya baridi.
6. MAGANDA YA MACHUNGWA
Warembo wangu hii itawafaa, kausha vizuri maganda ya machungwa kwa siku tatu juani.Yatwange au saga kutengeneza poda au ungaunga weka kwa kikopo na funika.Chota vijiko viwili changanya na rose water (inapatikana madukani) paka kwapani. Acha ikauke kwa dakika kumi halafu uoshe na maji baridi. Kwani bafuni tunaweka nini zaidi ya vitu kama hivi? Msimu wa machungwa haujaisha wapenzi.
7. MAZIWA
Wapenzi wa kunywa maziwa siwaoni wakifanya hii…ila ina majibu ya haraka ukifanya kila siku. Paka maziwa kidogo tu kwenye kwapa acha yakauke kwa dakika 15 halafu oga. Fanya hivi kila siku kupata majibu.
8. MAFUTA YA NAZI
Hakuna kitu ambacho mafuta ya nazi hayafanyi!!hata hivyo ni kiungo cha urembo duniani kote.Inafanya kazi taratibu.Hivyo nashauri utumie kila siku. Jisugue (massage) na mafuta ya nazi kwa dakika 15 kabla hujaoga.Wapenzi wa deodorant hii pia ni deodorant ya asili.
9. VINEGAR

Kama msomaji mzuri wa post zangu lazima uwe na vinegar nyumbani mpaka sasa. Ina matumizi mia kidogo, supermarket zote zipo.paka kwapani acha kwa dakika kumi then oga. Inaondoa harufu, inaua bacteria na inatoa weusi.
10.UNGA WA DENGU ( GRAM FLOUR )
Hii inasaidia pia kutoa mabaka ya chunusi, na weusi sehemu zote mwilini ikiwemo kwapa.Changanya na juisi ya limao na yogurt paka kwenye kwapa kila siku and watch the magic happen. Ni salama
11. APPLES.
Apple ina kiwango cha acid pia hivyo ukisugua kwapa na apple lililosagwa inatoa weusi na harufu. Fanya hivi angalau mara moja kwa siku kabla ya kuoga.
12. YOGHURT
Changaya yoghurt vijiko viwili na asali kijiko kimoja kisha paka kwenye kwapa acha ikauke , osha na maji baridi itasaidia kutoa uchafu na weusi kwenye kwapa.
Unaweza chagua njia moja kati ya hizi au unaweza changanya njia mbili kwa wakati mmoja, Njia zote ni salama sana na ni rahisi sababu vitu vyote hivi ni viungo na vyakula ambavyo tunatumia nyumbani. Kama una swali uliza kwenye comment au maoni na atakaejaribu njia yoyote atupe majibu yake kwa comments.
xoxo
chelly
image powered by google.






Thank you chelly......naenda kufanya....ntakupa majibu😃😃😃
ReplyDeleteAsante mamaa nimeona ubarikiwe
ReplyDeleteKama njia zote hizo ni sahihi na effective, then which one is the ultimate best??? + ngapi zimefanyiwa majaribio na kuhakikiwa? cuz ijapo vitu vyote hivyo ni asilia, am absolutely certain yakua kwa zake namna zina side effects pia unless pharmaceutical proven.
ReplyDeleteWell thank you for your input, kama ilivyoandikwa vitu vyote vilivyoandikwa ni vyakula na viungo asilia tunavyotumia nyumbani. Ni kiasi cha mtu kujaribu kipi kitamfaa, kamaa ana allergy na kiungo chochote asitumie.Kusema ipi ni nzuri mhhh thats quit difficult sababu our skin reacts different to certain product even though the content the same.Again most of these are from personal experience and reading from other sources.If you have a snsitive skin i would suggest umuone daktari wa ngozi. Thank you for visiting.
ReplyDeleteHello umesema naweza kutumia aina mbili as same time sasa natumiaje au mf. Asubuhi natumia limao jioni natumia tango?
ReplyDelete