Wednesday, August 9, 2017

JINSI YA KUONDOA HARUFU MBAYA MDOMONI HARAKA.

Image result for how to get good breath all the time
Bad breath, sote tunafahamu hili tatizo, sio dogo kama tunavohisi. Na  kila mtu ana harufu mbaya mdomoni inategemea tu na usafi wako wa kutunza kinywa chako. Ok kwa wale wenzangu na mimi kutwa mswaki lakini harufu ipo tu shida iko wapi? Fata tips hizi nyepesi ninazokupa baada ya wiki utanipa majibu ikshindikana muone daktari wa meno.

a) SAFISHA ULIMI VIZURI.
 

Watu wachache sana huchukua zaidi ya nusu dakika kusafisha ulimi, well siri ni kwamba ulimi unatunza sana uchafu katika kinywa, hivyo kuepuka harufu mbaya kama husafishi ulimi vizuri ni historia. Unaweza tumia kijiko kutoa uchafu au nunua tongue cleaner kwa bei nafuu pharmacy. Tuwafundishe watoto tabia hii mapema.

b.) TUMIA MOUTH WASH ZA ASILI NA DUKANI.
 

Njia nyingine rahisi ya kupata harufu nzuri au fresh breath ni kutumia maji ya chumvi kusuuza mdomo wako. Ni rahisi, haina gharama na haina madhara.Weka chumvi kwa glass ya maji sukutua .Ukiweza kununua mouthwash za dukani kama listerin ni vizuri pia.

c.) MDARASINI NA IRIKI
 
Hivi viungo vinatumika toka kale na wahenga kuweka harufu nzuri mdomoni.Ukila vyakula vyenye viungo vingi au ukihisi mdomo haueleweki chukua punje ya iriki au kipande cha mdarasini tafuna.Ukiweza chemsha maji ya viungo hivi na sukutua.

d.) APPLE, TANGO NA PERA.
 
 
 Matunda kama haya yanaongeza mate mdomoni na kuzuia uwepo wa bacteria ambao husababisha harufu mbaya. Kula kipande cha tango au apple hasa baada ya chakula. Pera husaidia wale wanaotoka damu kwenye fizi pia.

e.) VINEGAR
 
 Tumia vinegar ya apple inaweza saidia kupunguza uzito pia.Changanya vijiko viwili  vya vinegar na glass ya maji halafu kunywa. Au pia waweza sukutua kama mouthwash.

f.) KUNYWA MAJI MENGI NA GREEN TEA 
 

Ili kuzuia mdomo kukauka hali ambayo husababisha  ukuaji wa bacteria mdomoni na husababisha harufu mbaya jitahidi kunywa maji mengi na green tea kila siku.


 Hakuna gharama katika njia hizi, vingi ni vitu tunavotumia nyumbani kama viungo na chakula.so why not try today? Share your feedbacks with us.

 karibuni,
Chelly.



image powered by google
 
    
  





 

Share:

6 comments:

  1. Ooooh dat's nice ....nimepata somo thanks Cc'

    ReplyDelete
  2. nikitoa harufu mbaya mdomoni tena ni uzembe sasa.....ahsante

    ReplyDelete
  3. So ukitafuna tango mara kwa mara hyo issue ya Harufu hupotea...

    ReplyDelete
    Replies
    1. yes pamoja na kuzingatia kanuni bora za usafi wa meno. Isipoacha nashauri uonane na daktari wa meno.

      Delete

Search This Blog

Chaila Mustapha. Powered by Blogger.

Recent Posts

Theme Support